Lissu afikishwa Mahakamani Dar es Salaam
2 Juni 2025Matangazo
Katika hatua nyingine, Mahakama ya Tanzania imetangaza kwamba mwenendo wote wa mashauri hayo utarushwa mubashara kwa umma kupitia mitandao rasmi ya Mahakama.
Mahakama hiyo imesema lengo la kuirusha mubashara kesi hiyo ni kuwawezesha wananchi kuweza kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani kwa sababu Mahakama ya Kisutu inao uwezo wa kuchukua watu 80 pekee.
Hatma ya makada wa CHADEMA waliojiondoa yazua mjadala pana
Inafaa kukumbuka kwamba Lissu alitiwa hatiani kwa kudai marekebisho katika mifumo ya uchaguzi nchini Tanzania ambapo hata hivyo chama chake cha CHADEMA tayari kimeondolewa kwenye uchaguzi wa urais na ubunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.