Libya: Hatuna makubaliano na Marekani kuhusu wahamiaji
8 Mei 2025Matangazo
Serikali hiyo imesema pia, inapinga vikali uwepo wa makazi mapya ya kudumu ya wahamiaji katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.
Vyombo kadhaa vya habari vya Marekani viliripoti mapema mwezi Mei kwamba utawala wa Rais Donald Trump unapanga kuwapeleka wahamiaji waliofukuzwa kutoka nchini humo katika nchi za Libya na Rwanda.
Serikali ya Rwanda ilithibitisha kuwa katika mazungumzo ya awali na utawala wa Trump kuhusu kuwapeleka nchini Rwanda wahalifu waliokamilisha adhabu zao magerezani nchini Marekani.