Leverkusen yamsajili winga mwenye kasi Poku
12 Agosti 2025Haya yamesemwa Jumanne na klabu hiyo.
Kulingana na ripoti, Leverkusen italipa karibu yuro milioni 10 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.
"Ernest Poku ni mchezaji mzuri sana ambaye kasi yake na uwezo wake wa kuchenga utatoa mchango wa kipekee kwa safu yetu ya ushambulizi," alisema Simon Rofles, mkurugenzi mkuu wa michezo wa Leverkusen.
Poku anatarajiwa kuichukua nafasi ya Jeremie Frimpong ambaye alijiunga na Liverpool kama kiungo mbunifu Florian Wirtz. Leverkusen pia waliwapoteza kiungo mkabaji Granit Xhaka, Beki Jonathan Tah na mlinda lango Lukas Hradecky pamoja na kocha wao Xabi Alonso.
Kufikia sasa klabu hiyo imefanya usajili wa viungo Ibrahim Maza na Malik Tillman, beki Jarell Quansah na walinda lango Mark Flekken na Janis Blaswich.