Leverkusen na Bayern kuumana katika mechi muhimu
14 Februari 2025Mtanange huo wa timu mbili zilizoko kileleni pia ni mnyukano kati ya vijana wawili matata sana wa Kijerumani ambao ni Florian Wirtz wa Leverkusen na Jamal Musiala wa Bayern.
Bayern inaingia kwenye mechi hiyo ikiwa usukani na pengo la point inane dhidi ya Leverkusen waliobeba ubingwa wa msimu wa 2023-24 kwa mara yao ya kwanza na kuiwekea kikomo rekodi ya Bayern kubeba taji kwa miaka 11 mfululizo.
Mjumbe wa bodi ya Bayern anayehusika na michezo Max Erbel amewaambia waandishi kuwa hawawazi tu kuhusu Leverkusen ambao hawajawashinda katika mechi tano.
"Sio tu kuhusu mechi moja au mbili bali msimu mzima. Tunakata kushinda kila mechi. Sio kuwanyamazisha Leverkusen katika mechi hii, bali ni kushinda kila mchuano.
Bayern wanaingia katika mechi hii wakiwa wameshinda mechi saba mfululizo wakati Leverkusen imeangusha pointi kutokana na sare dhidi ya RB Leipzig na Wolfsburg baada ya mapumziko ya msimu wa baridi.
Wirtz v Musiala
Akiwazungumzia Wirtz na Musiala, kocha wa Bayern Vincent Kompany amesema kuwa "kandanda la Ujerumani linapaswa kufurahishwa kuwa wote wanaichezea timu ya taifa. "haupaswi kutafuta sana tofauti baina yao au kuuliza nani ndiye bora. Wote ni wachezaji bora zaidi. Ni vizuri kuwa nao kwenye ligi moja, na timu moja ya taifa. Nadhani wanaweza kuimarika hata zaidi.” Amesema Kompany.
Musiala amesaini mkataba mpya na Bayern Munich hadi Juni 2030. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anayechezea timu ya taifa ya Ujerumani alijiunga na Bayern mwaka wa 2019 akitokea akademi ya Chelsea.
katika klabu ya Bayern na kumekuwepo na tetesi kuwa Bayern katika siku za usoni huenda ikamnyakuwa Wirtz ambaye ana mkataba na Leverkusen hadi 2027.
dpa