Leverkusen hatimaye wakubali kumuuza Wirtz kwa Liverpool
13 Juni 2025Maombi mawili ya Liverpool yalikataliwa ombi la mwisho likiwala pauni milioni 113 ambapo pauni 100 zingelipwa kwa pamoja kisha hizo fedha za ziada zikaongezeka kulingana na ufanisi ambao angeupata Wirtz hapo Liverpool, ila kwa sasa makubaliano yameafikiwa.
Bado Liverpool watalipa pauni milioni 100 kama ada ya awali kisha hizo pauni milioni 16 zilizosalia zitalipwa baadae na hivyo kumfanya Wirtz kuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa bei ya juu zaidi huko Uingereza.
Leverkusen walikuwa wamemuwekea Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 22 bei ya pauni milioni 125 ila hata Liverpool wakilipa hizo pauni milioni 116, watakuwa wameikivuka kiasi cha pauni milioni 115 wambazo Chelsea waliwalipa Brighton & Hove Albion kwa ajili ya saini ya Moises Caicedo.
Mshambuliaji wa Liverpool Darwin Nunez ndiye aliyekuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa kiwango cha juu cha fedha na Liverpool kabla Wirtz, ila hao the Reds hawajazilipa kikamilifu pauni milioni 85 ambazo Benfica walikuwa wanataka kwa kuwa Nunez hajatimiza malengo aliyokuwa amewekewa ili fedha hizo kulipwa.