SiasaLesotho
Lesotho yafedheheshwa na tamko la Trump la kutoitambua
6 Machi 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lesotho, Lejone Mpotjaone amesema amemwalika kiongozi huyo wa Marekani kuitembelea nchi hiyo.
Siku ya Jumanne Trump akihutubia bunge la nchi yake aligusia juu ya msaada wa Marekani unaotolewa kwa nchi za kigeni, akisema kwamba dola milioni 8 zinatolewa na nchi hiyo kuunga mkono harakati za watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja katika taifa la Lesotho, barani Afrika ambalo hakuna anayelitambua.
Waziri wa mambo ya nje wa Lesotho ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kauli hiyo ya Trump ni matusi na kebehi kwa taifa lake.