Le Pen azuiwa kuwania uchaguzi kwa miaka mitano
1 Aprili 2025Matangazo
Mwanasiasa huyo mwenye utata ameapa kuikatia rufaa na kutoachana na azma yake ya kupigania urais mwaka 2027.
Hukumu hiyo ni sehemu ya mkururo wa maamuzi mengine juu ya hatia ya kuunda ajira za uongo kwenye Bunge la Ulaya kwa niaba ya chama chake cha National Rally, mashitaka ambayo Le Pen ameyakanusha vikali. Hukumu hiyo imekosolewa pia na Ikulu ya Urusi, Kremlin, bilionea wa Marekani, Elon Musk, na wanasiasa wa mirengo mikali ya kulia barani Ulaya, akiwema Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, na Geert Wilders wa Uholanzi.