Le Pen angojea hukumu ya ubadhirifu wa euro milioni saba
31 Machi 2025Matangazo
Kwenye kesi hiyo, chama hicho kinatuhumiwa kupokea fedha kutoka Bunge la Ulaya kwa ajili ya malipo ya wasaidizi wa bunge, ambao walikuwa ama ni wafanyakazi wa muda au wa kudumu wa chama chake.
Jumla ya watuhumiwa wengine 28 wamejumuishwa kwenye kesi hiyo ya ubadhirifu wa euro milioni saba, ambayo hukumu yake itaamua mustakabali wa kisiasa wa Le Pen na chama chake.
Mwanasiasa aliwahi kurejesha euro 300,000 mnamo mwaka 2023, lakini chama chake kinasema malipo hayo hayakumaanisha kukiri makosa. Endapo hukumu ikiwa dhidi yake, huenda Le Pen akazuiwa kuwania uchaguzi ujao mwaka 2027.