Wahariri wa magazeti ya Ujerumani katika maoni waliyoyachapisha leo wanaiunganisha siasa ya ndani na siasa ya nje. Jana mwenyekiti wa chama cha Social Democrats, Kurt Beck, alijibu swali vipi anataka kushinda katika uchaguzi ujao. Wakati huo huo serikali ya Ujerumani bado haijaamua kuhusu mchango wake katika operesheni ya kijeshi ya kimataifa huko Mashariki ya Kati.