Lavrov na Rubio kukutana Riyadh kuijadili Ukraine
17 Februari 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov atakuwa na mazunngumzo na mwenzake wa Marekani Marco Rubio pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa pande hizo mbili mjini Riyadh kesho Jumanne.
Mazungumzo hayo yanafanyika baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwasiliana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wiki iliyopita na kuwaamuru maafisa wao kuanza majadiliano ya kumaliza vita vinavyoendelea.
Soma pia:Trump atangaza kukutana na Putin siku za usoni
Hata hivyo Ukraine haitowakilishwa kwenye mazungumzo hayo ya Riyadh, na kiongozi wa nchi hiyo Volodymyr Zelenskiy amesema hawatayakubali matokeo ya mkutano wowote utakaojadili kumaliza vita bila ya Ukraine kuhusishwa.