Lavrov akutana na mwenzake wa Korea Kaskazini
12 Julai 2025TASS, imemnukuu Lavrov akisema kuwa walibadilishana mawazo juu ya hali inayozunguka mgogoro wa Ukraine na kwamba rafiki zao wa Korea wamethibitisha kuhusu msaada wao thabiti kwa malengo yote ya operesheni hiyo maalumu ya kijeshi, pamoja na vitendo vya uongozi wa Urusi na vikosi vya kijeshi.
Marekani na washirika wazituhumu Urusi, Korea kaskazini kukiuka vikwazo vya UN
TASS, pia imemnukuu naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Andrei Rudenko akisema kuwa wajumbe zaidi wa ngazi ya juu watafanya ziara Korea Kaskazini baadaye mwaka huu.
Rudenko amesema makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati, unakidhi mahitaji yanayobadilika katika miongo ya hivi karibuni na kuimarisha urafiki wa jadi kati ya mataifa hayo mawili kufikia kiwango kipya cha ubora kama washirika.