Latvia yajiondoa kwenye mkataba unaopinga mabomu ya ardhini
17 Aprili 2025Matangazo
Wabunge nchini Latvia wamepiga kura kuiondowa nchi hiyo kwenye mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya mabomu ya ardhini.
Hatua ya Latvia ambayo inapakana na Urusi imechukuliwa kwa lengo la kuimarisha usalama wake chini ya kiwingu cha vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Nchi hiyo ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya kujihami ya NATO pamoja na mataifa mengine kwenye kanda hiyo, wameimarisha bajeti zao za ulinzi na utoaji mafunzo ya kijeshi tangu Moscow ilivyopeleka vikosi vyake Ukraine mwaka 2022.
Mataifa hayo yanakhofia kwamba Urusi huenda ikayalenga baada ya kuisambaratisha Ukraine.Mkataba wa Ottawa,unaokataza matumizi ya mabomu ya ardhini,umetiwa saini na nchi 160 isipokuwa Marekani na Urusi.