Lagos:Kituo cha polisi chavamiwa.
18 Agosti 2006Matangazo
Watu wenye silaha amekishambulia kituo cha Polisi katika maeneo ya ya mji wa bandari wa Harcourt wenye mafuta na kuwauwa kuwauwa maafisa watatu na kuwajeruhi kadhaa.
Akilizungumzia tukio hilo mrakibu muandamizi wa polisi amesema Shambulio hilo lililofanyika mapema jana lilikuwa ni la kustukiza, wakati kundi hilo la wahalifu walipokivamia kituo cha Ahoada na kupiga risasi.
Hakuna yeyote hadi hivi sasa aliyekamatwa kufuatia tukio hilo lakini uchunguzi unaendelea katika eneo hilo la tukio.