LA PAZ Maandamano yafanyika nchini Bolivia
1 Juni 2005Matangazo
Polisi wa kuzima fujo nchini Belarus wamekabiliana na waandamanaji katika mji mkuu La Paz. Maelfu ya waandamanaji walikusanyika mjini humo hapo jana wakitaka kutaifishwa kwa sekta ya nishati nchini humo. Polisi wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamaji hao, ambao baadhi yao waliendelea kuwa wakaidi na kuchoma matairi na kuripua baruti zinazotumiwa kwenye migodi.
Shina kubwa la mandamano hayo ni nishati ya gesi nchini humo ambayo inachukua nafasi ya pili huko Amerika Kusini kwa ukubwa. Raia wanataka nao wafaidi kutokana na nishati hiyo. Asilimia kubwa ya viwanda vya mafuta na gesi nchini Bolivia vinamilikiwa na makampuni kutoka mataifa ya kigeni.