Kwanini Pakistan inawafukuza wakimbizi wa Afghanstan?
26 Februari 2025Mnamo mwaka 2023 Pakistan ilianzisha mpango mkubwa wa kuwarejesha nyumbani takriban Waafghani milioni 4 ambao wameingia nchini humo katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.
Mwaka uliopita mamlaka iliwaruhusu kuendelea kusalia kwa muda. Serikali ya Pakistani sasa imeweka mpaka Machi 31 raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume na sheria kuondoka, huku msako ukiendelea katika kipindi cha mwezi Januari na Februali.
Mtaalamu wa sheria na mwanaharakati wa masuala ya haki za wakimbizi Umer Gillani ameiambia DW kwamba wakimbizi wa Afghanistan wanaoishi Islamabad na mji mwingine wa Rawalpindi wametakiwa kuondoka Pakistan hadi kufikia Februari 28 na kuongeza kuwa tangazo hilo linaongeza hofu na kutokuwa na uhakika miongoni mwa Waafghanistan katika eneo hilo.
Mwanaharakati huyo ameendelea kuiambia DW kwamba tangu kuanza kwa mwaka huu zaidi wa Waafganistai elfu moja wamezuiliwa katika mji wa Islamabad huku wengine zaidi ya elfu kumi na nane wamelazimika kuondoka Islamabad na Rawalpindi kufuatia amri hiyo ya serikali.
Soma pia:Taliban yataka Waafghani walio Pakistan wasaidiwe
Hivi karibuni polisi wakiwemo maafisa wa kike walifanya upekuzi kwenye majengo ya makaazi wakiwasaka wakimbizi wa Afghanistan wasio na vibali na kuwakamata baadhi.
Mwanaharikati wa haki za binadamu Rahil Talash amesema kuwarudisha Afghanista ni kuwarejesha kwenye hatari "wale waliokimbia Afghanistan baada ya 2021 walifanya hivyo kwa sababu maisha yao yalikuwa hatarini."
Aliongeza kwamba wakimbizi hao walitafuta usalama nchini Pakistan, lakini badala yake, wanakabiliwa na kufukuzwa.
"Huu ni ukiukwaji wa wazi wa kanuni za kibinadamu.Mtu ambaye amekimbia kulinda maisha yake sasa anarudishwa kwenye hatari ile ile, ambayo ipo kwenye hatma ya Taliban."
Kuzorota kwa mahusiano baina ya Pakistan na Taliban
Mahusiano baina ya Pakistan na jirani yake Afganistan yamezoroa kwa miaka mitatu sasa, Islamad ikishikilia msamamo wake ikitaka utawala wa Taliban nchini Afganistan kuwajibika kwa kushindwa kudhibiti oparesheni za kundi la wanamgambo wa Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP) ambalo limefanya mashambulizi mengi dhidi ya vikosi vya usalama vya Pakistani.
Huku mvutano baina ya pande mbili ukizidi kuongezeka, pia wasiwasi umeibuka kufuatiwa kuwepo kwa ripoti za kutishwa na kukamatwa kwa Waafghanistan.
Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake na kuongeza kwamba Waafghanistan katika eneo hilo wanastahili kutendewa haki, huku mwanaharakati wa haki Gilan akiiambia DW mamilioni ya wakimbizi wa Afghanistan nchini Pakistan wanatumiwa kama "mateka kujenga shinikizo kila kunapokuwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili.
Soma pia:Waafghani wanaofukuzwa Pakistan wakabiliwa na madhila makubwa
Wizara ya mambo ya Nje nchini Pakistan juma lililopita ilitupilia mbali madai yaliyotolewa na wawakilishi wa Afghanistan juu ya kunyanyasika kwa wakimbizi wa Afghanistan nchini Pakistan na kuyataja madai hayo "hayana mashiko" na kuitaka Kabul kuwezesha kuwarejesha makw ao raia wa Afghanistan.
Baada ya Taliban kutwaa madaraka mnamo Agost 2021, maelfu ya Waafganistan walivuka mpaka na kuingia Pakistan, wakitegemea kuongezewa viza kila wakati ili kuendelea kubakia nchini humo.
Hata hivyo mchakato huo unatajwa kuwa ni gaharama kubwa, wenye changamoto nyingi na mara nyingi inakabiliwa na ucheleweshaji.
Wanaharakati wa haki za binadamu katika eneo hilo wanasema tangazo la mamlaka ya Pakistan lipo nyuma ya shinikizo la kisiasa, kufuatia mvutano baina ya mamlaka za nchi.