Mwanasiasa wa chama cha Christian Democratic Union, CDU, Joe Chialo, ambaye alikuwa waziri wa utamaduni na masuala ya kijamii wa jimbo la Berlin amejiuzulu wadhifa wake baada ya kutumikia kwa zaidi ya miaka mitatu. Hawa Bihoga amezungumza na mwanasiasa huyo mwenye asili ya Tanzania na kwanza alitaka kujua sababu kuu ya kujiuzulu kwake.