Kwa nini EU inakwepa kulaani ukandamizaji wa Uturuki?
17 Aprili 2025Siku ya Ijumaa, Meya wa mji wa Istanbul, Uturuki Ekram Imamoglu alifika mahakamani katika moja ya kesi nyingi dhidi yake zinazomkabili huku wafuasi walikusanyika kupinga kile wanachoamini kuwa ni kampeni iliyochochewa kisiasa ya kumzuia kuwania urais.
Maelfu ya waandamanaji waingia barabarani Istanbul
Mbali na hilo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanahoji kwanini umoja wa ulaya unakwepa kulaani ukandamizaji wa kisiasa nchini Uturuki?
Mpinzani mkuu wa Rais Recep Tayyip Erdogan yuko gerezani
Ekrem Imamoglu, ambaye amekuwa akishikiliwa katika gereza la Silivri tangu Machi 23, ndiye mgombea urais wa chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki cha CHP na anayeonekana kama mgombea aliye na nafasi nzuri zaidi ya kumshinda Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye amekuwa mamlakani kwa takriban robo karne.
Mashtaka dhidi ya Imamoglu yadaiwa kuchochewa kisiasa
Kifungo cha Imamoglu kimetazamwa na watu wengi kuwa kilichochochewa kisiasa, lakini serikali ya Erdogan inasisitiza kwamba mahakama iko huru na haina ushawishi wa kisiasa. Ikiwa atahukimiwa, Imamoglu anaweza kupigwa marufuku kuingia katika ofisi ya umma.
Kamata kamata yaendelea Uturuki dhidi ya maelfu ya waandamanaji
Lakini licha ya wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali na kesi ambayo wengi wanaona kuwa ni hatua nyingine ya Uturuki kuingia katika utawala wa kimabavu, jibu la Umoja wa Ulaya limeonekana kutokuwa na mashiko.
Viongozi wa EU hawako tayari kuonekana kuwa na chuki na Erdogan
Selim Kuneralp, balozi wa zamani wa Uturuki katika umoja wa ulaya, aliiambia DW kwamba EU imekuwa "inasita kidogo" kujibu kukamatwa kwa meya na ukandamizaji uliofuata dhidi ya waandamanaji. "Nafikiri viongozi wa Umoja wa Ulaya hawakuwa tayari kuonekana kuwa na chuki sana na Rais Erdogan," aliongeza.
Uturuki inataka kujiunga na Umoja wa Ulaya
Uturuki ni nchi inayotaka kujiunga na Umoja wa Ulaya na inayotarajiwa kuwa na viwango vya juu zaidi katika utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.
Erdogan ataka chama cha PKK kuvunjwa mara moja
Lakini kuongezeka kwa thamani ya kimkakati ya Uturuki kama mwanachama wa NATO, wataalam wanasema, inaonekana kuwa imeathiri mwitikio wa Ulaya kwa kuzorota kwa maadili haya.
Baraza la Ulaya, taasisi inayoongoza masuala ya haki za binadamu limetoa wito wa "kuachiliwa mara moja" kwa meya. Na baadhi ya wanasiasa wakuu nchini Ujerumani ambayo ina idadi kubwa ya waturuki pia wameonyesha kuunga mkono waandamanaji.
Mwanasiasa wa Ujerumani atilia shaka uhuru wa mahakama
Felix Banaszak, mwenyekiti mwenza wa Chama cha Kijani cha Ujerumani, alitembelea Uturuki ili "kuunga mkono nguvu za kidemokrasia."Serpil Midyatli, naibu kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Social Democratic Party (SPD) nae alionyesha wasiwasi wake juu ya uhuru wa mahakama na kama meya atapata haki kwenye kesi yake inayomkabili.
Serpil anasema "tayari kuna dalili zaidi ya moja kwamba mahakama haiko huru tena," aliiambia DW siku ya Ijumaa, akiongeza kuwa kesi hiyo inaweza "kuburuzwa kwa muda mrefu iwezekanavyo."
Kamishna wa EU asusia ziara ya Uturuki
Marta Kos, Kamishna wa Umoja wa Ulaya wa upanuzi na ambaye pia anawajibika moja kwa moja kwa Uturuki kujiunga na umoja huo, alighairi ziara ya Uturuki kupinga kukamatwa kwa meya. Alitakiwa kuhudhuria Kongamano la Diplomasia la Antalya, lililopangwa kufanyika Aprili 11-13, na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan.
Maandamano ya Uturuki yalenga kudhibiti madaraka ya Erdogan
Hata hivyo, EU haijatoa maoni mengi zaidi kuhusu kuzuiliwa na kukamatwa kwa Meya wa Istanbul Ekrem Imamoglu na watu wengine mashuhuri, wakiwemo wanahabari na wawakilishi wa mashirika ya kiraia," alisema Kos katika Bunge la Ulaya mjini Strasbourg mnamo Aprili 1, na kuyataja kuwa ni matokeo ya "kurudi nyuma kidemokrasia."
Lakini je, Uturuki ni muhimu kwa usalama wa Ulaya?
Kama sehemu ya makubaliano ya 2015 ambayo Uturuki ilipokea euro bilioni 9 katika muongo uliopita, na ikaahidi kupunguza uhamiaji usio wa kawaida katika EU. Na miezi minne tu iliyopita, ilipata ushindi wa kisiasa wa kijiografia wakati waasi wanaoungwa mkono na Uturuki walipomwondoa madarakani Rais wa Syria Bashar Assad na kuunda serikali ya mpito mwezi Desemba.
Labda muhimu zaidi kutoka kwa mtazamo wa usalama wa Ulaya, Uturuki imedumisha uhusiano wa karibu na Urusi tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine.Kuna hisia inayoongezeka kwamba Istanbul inaweza kuhitaji kuchukua jukumu ili kudumisha amani, mara tu itakapoanzishwa.
"Usalama wa Ulaya haufikiriki bila Uturuki,"Rais Erdogan alisema hivi majuzi alipokuwa akitetea ushirikiano wa kina na nchi za Ulaya.
Mkuu wa NATO ahepa swali kuhusu kukamatwa kwa Imamoglu
Katika mkutano na waandishi wa habari mapema mwezi wa Aprili, Mkuu wa NATO, Mark Rutte alikwepa swali kuhusu kukamatwa kwa Imamoglu alipoulizwa iwapo NATO itatafakari upya pendekezo la Uturuki la kuwa mwenyeji wa washirika hao kwa mkutano usio rasmi uliopangwa kufanyika mwezi Mei.
Poland yatamani Uturuki ichukue jukumu katika kumaliza vita Ukraine
Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk amesema anatamani Uturuki ichukue nafasi kubwa katika kumaliza vita nchini Ukraine, na kujadili "pendekezo la wazi kwa Uturuki kuchukua jukumu kubwa zaidi la ushirikiano" kutatua mzozo huo.
Takriban waandamanaji 1,100 wakamatwa na polisi Uturuki
Tangu kuanza kwa vita mnamo Februari 2022, Uturuki imekataa kuweka vikwazo dhidi ya Urusi na kuendelea kununua nishati ya Urusi ambayo imechochea mitambo ya vita ya Kremlin.
Na wengine wanahofia utegemezi wa kiuchumi wa Uturuki kwa Urusi huenda ukaiweka karibu na Moscow kuliko Ulaya.