Wataalamu nchini Japan wanafanya juhudi za kutengeneza maroboti yenye tabia zinazofanana na binadamu yenye uwezo wa kufanya kazi katika huduma za afya hasa kwa wazee wasiojiweza. Ni wakati nchi hiyo ikikabiliwa na uhaba wa kazi huku kukiwa na idadi kubwa ya wazee.