Joanitha ni mwanafunzi anayesomea masuala ya ustawi wa jamii. Amekuwa msichana anayepinga masuala ya rushwa ya ngono kwa wasichana pamoja na wanawake. Anatumia nafasi yake kama msichana katika jamii kutoa elimu kwa wasichana na wanawake, ili kuhakikisha kuwa msichana anapata haki yake bila kikwazo chochote.