Kushuka kwa uchumi wa Ujerumani ni angalizo
15 Agosti 2019Sekta ya viwanda ya Ujerumani ambayo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wan chi hiyo imeanza kuporomoka. Makampuni mengi zaidi yanapunguza uzalishaji wakati ambapo sababu kubwa inatajwa kuwa ni migogoro ya kibiashara lakini pia sababu nyingine inaelezwa kuwa ni mabadiliko na mgogoro unaozzidi kufukuta katika sekta ya utengenezaji magari. Pia uwezekano wa Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya bila makubaliano pamoja na maandamano makubwa mjini Hong Kong, vinasababisha mchanganyiko unaotishia kuharibu mipango ya biashara.
Ingawa kushuka huku kwa uchumi kunasababishwa zaidi na mambo ya nje ya taifa hilo, haya matokeo ya biashara za kawaida kupoa baada ya kupanuka kwa miaka nane nchini Ujerumani. Mzunguko wa biashara ni jedwali lenye kupanda na kushuka na si mstari ulionyoka ambao huenda juu muda wote.
Nini kifanyike kudhibiti kuporomoka zaidi kwa uchumi wa Ujerumani?
Jambo litakalosaidia kuondoa mdororo huu wa uchumi ni kupunguza kwa kasi kodi ya mapato kwa waajiriwa. Ni wakati sasa wa waziri wa fedha kufungua mkoba wa serikali, ili kuwafanya wajerumani watumie na kununua zaidi.
Nyakati kama hizi hakuna anayehitaji sifuri nyeusi ambazo zimekuwa alama ya mafanikio ya Ujerumani katika kuleta usawa kazi ya matumizi ya nchi na bajeti. Pamoja na hayo, hakuna hofu ya watu kupoteza vibarua vyao, waau kwa sasa. Hapana shaka kuwa inatisha kusikia habari toka kwa makampuni makubwa kama vile Bayer, BASF na Volkswagen ambayo yametangaza kupunguza wafanyakazi.
Lakini makampuni hayo hayawakilishi uchumi wote wa Ujerumani bali maelfu ya biashara dogo na za kati ambazo zilitengeneza nafasi za kazi zilizochochea ongezeko la ajira nchini Ujerumani kwa miaka kadhaa iliyopita.
Kinachohitajika hivi sasa ni mawazo mazuri kama alile ambalo lilitolewa na mchumi wa Ujerumani Michael Hüther. Ametaka kuundwa kwa mfuko maalumu wa Ujerumani wenye thamani ya Euro bilioni 450 zitakazotakiwa kutumika ndani ya miaka 10 ijayo.
Mfuko huo unaweza kupata fedha kupitia mtaji wa masoko ambapo wawekezaji wamedhamiria kulinunua deni la Ujerumani na kuwekeza kwa kukubali hatari ndogo ya kufilisika kwa biashara zao. Fedha hizi ni kwa ajili ya madumuni mbalimbali kama vile usafiri wa jumuiya, huduma ya mtandao yenye kasi, makazi, elimu na kulinda mazingira.
Mwandishi: Henrick Böhme
Tafsiri: Angela Mdungu