Kurunzi Wanawake leo inamuangazia daktari Maryam Badawy ambaye ameingia kwenye historia katika tasnia ya tiba kwa kuwa mwanamke wa kwanza katika eneo la pwani ya Kenya kuwa daktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile. Daktari Maryam amekuwa alama ya matumaini kwa wanawake wanaopambana na saratani ya matiti.