Ulimwengu leo unaadhimisha siku ya kusikia duniani. Utafiti uliofanywa na shirika la afya duniani WHO umeonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 400 wanahitaji msaada wa kuwezeshwa kusikia. Wataalam wa afya wametahadharisha juu ya kusikiliza muziki kwa sauti kubwa na kwamba tatizo la watu kutosikia linaendelea kukua kwa kiwango cha kutia wasiwasi.