SiasaKorea Kusini
Lee Jae-myung atabiriwa kushinda uchaguzi wa urais
3 Juni 2025Matangazo
Wakati tayari asilimia 78 ya kura ikiwa imehesabiwa, Lee anaongoza kwa asilimia 51.7, akifuatiwa na mpinzani wake kihafidhina, Kim-moon Soo, mwenye asilimia 39.3.
Msemaji wa chama cha Lee cha Democratic amewasifu wapiga kura kwa kuiadhibu vikali serikali iliyopita, huku msemaji wa chama cha kihafidhina cha PPP akielezea mshituko kufuatia matokeo hayo.
Karibu Wakorea Kusini milioni 44.4 wanapiga kura kwenye uchaguzi huo wa mapema wa rais, uliochochewa na kuondolewa madarakani kwa Yoon Suk Yeol, kufuatia jaribio la kuanzisha sheria ya kijeshi Disemba iliyopita.