Kura ya Poland Jumapili kuamua mkondo itakaochukuwa nchi
30 Mei 2025Matangazo
Haya yanafanyika huku tafiti za maoni zikitabiri ushindani mkali katika uchaguzi utakaofanyika Jumapili.
Uchaguzi huo ndio utakaoamua mkondo itakayochukua nchi hiyo muhimu ya Umoja wa Ulaya na mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.
Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kwamba Trzaskowski atapata asilimia 50.6 ya kura huku asilimia 49.4 ya kura zikimwendea Nawrocki.
Ushindi kwa Trzaskowski utakuwa umeipiga jeki serikali ya Poland ambayo imekuwa katika mkwamo wa kisiasa na rais wa sasa.
Ushindi wake pia utamaanisha mabadiliko makubwa katika masuala ya kijamii kama kuhalalishwa kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja na kulegezwa kwa marufuku ya uavyaji mimba nchini Poland.