Kura ya Kombe la dunia 2006 Ujerumani
8 Desemba 2005Makocha wa timu zote 32 wameshawasili Leipzig pamoja na wale wa timu 5 za Afrika-Angola,Ghana,Ivory Coast,Togo na mabingwa wa Afrika Tunisia.Kura hii katika ukumbi mpya wa biashara wa Leipzig, itaongozwa na mrembo wa mavazi wa Ujerumani Heidi Klum. Wajumbe 500 kutoka FIFA wanahudhuria pia.
Kiasi cha mashabiki milioni 320 katika nchi 145 mbali mbali wanatazamiwa kuangalia tukeo hili .
Kura itachukua mfumo huu wa kijiografia ukizingatia kanda zote za dunia:Makundi yote 8 yatajumuisha si zaidi ya timu 2 kutoka Ulaya na hakuna kundi lolote litaloingiza zaidi ya timu 1 kutoka shirikisho la kanda nyengine .
Kanuni hii ilizusha matatizo katika kutunga makundi haya hapo kabla:Jumaane,timu ziligawanya makundi 3 ya timu 8.Chungu kimoja kikiingiza timu 1tu-Serbia na Montenegro na kundi 1 la timu 7.
Timu 32 zinazoania Kombe la dunia 2006 zimegawanywa hivi kwa madhumuni ya kupigiwa kura:Katika chungu cha kwanza:wako wenyeji Ujerumani,Brazil-mabingwa wa dunia,Uingereza-mabingwa 1966,Spain,Mexico,Ufaransa,mabingwa 1998 na Argentina,mabingwa x2 wa dunia halafu Itali mabingwa x3 wa dunia.Hizo ni timu zitakazoongoza kileleni makundi 8 ya kupigiwa kura:
Chungu 2:kitajumuisha timu za Afrika,America Kusini na eneo la Oceania:yaani angola,Ivory Coast,Ghana,Togo,Tunesia,Ecuador,Paraguay,na Australia.
Chungu cha 3:kuna timu za Ulaya:Croatia,Jamhuri ya Czech,Holland,Poland,Ureno,Sweden,Uswisi na Ukraine.
Halafu kutakua na chungu kimoja maalumu kikingiza timu moja tu- Serbia na Montenegro-zamani Yugoslavia.
Chungu cha 4:kina timu za bara la Asia,America kaskazini na Kati na nchi za bahari ya Karibik:
Nchi kama vile Iran,Japan,Korea Kusini,Saudi Arabia,Costa Rica,Marekani,Trinidad na Tobago.
Ili kuhakikisha pasiwepo timu 3 za Ulaya katika kundi moja,Jamhuri ya Serbia na Montenegro itapigiwa kura katika kundi moja na nchi isio ya Ulaya kutoka chungu cha I kinachojumuisha timu kama Brazil,Argentina au Mexico.
Baada ya kila timu imetiwa chungu chake kwenda chungu chengine,kura ya pili itapigwa kuamua mahala pa timu hiyo katika kundi lake.
Ujerumani kama mwenyeji,itawekwa kundi la AI wakati mabingwa Brazil wataangukia kundi FI.Mfumo huu utahakikisha kuwa timu hizi mbili zitacheza mechi zao za duru ya kwanza katika viwanja vikubwa na mashuhuri.
Timu 2 zitakazoibuka kutoka kila kundi-yaani ya kwanza na ya pili, ndizo zitakazoingia duru ya pili ya kutoana.
Watakaoongoza burdani hii ya dimba jioni hii ni rembo wa mavazi wa kijerumani, Heidi Klum akishirikiana na muandishi-habari wa michezo wa TV Reinhold Beckmann.Kura yenyewe ya bahati nasibu itaongozwa na mkurugenzi wa mawasiliano wa shirikisho la dimba ulimwenguni-FIFA-Markus Sieger.