KUNDUS: Vikosi vya Ujerumani vyatembelewa Afghanistan
19 Julai 2006Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amevitembelea vikosi vya Ujerumani na tume zinazosaidia kuijenga upya Afghanistan.Hivi karibuni,vikosi vya Ujerumani vilipewa dhamana ya kuongoza majeshi ya kimataifa yanayolinda amani-ISAF-kaskazini mwa Afghanistan.Tangu miezi michache ya nyuma,hali ya usalama imezidi kuwa mbaya katika eneo hilo na hata vikosi vya Kijerumani vimelengwa katika mashambulio ya waasi.Hivi sasa,Ujerumani ina wanajeshi 1,000 kaskazini mwa Afghanistan na idadi hiyo itaongezwa mwishoni mwa mwaka kufikia 1,400.