MigogoroMashariki ya Kati
Hamas yalitafakari pendekezo la kusimamisha mapigano Gaza
4 Julai 2025Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa 04.07.2025, hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya kundi hilo ili kuumaliza uchokozi wa Israeldhidi ya watu wake na kuhakikisha misaada ya kiutu inaingia Ukanda wa Gaza. Limeongeza kuwa litatoa uamuzi wa mwisho kwa wasuluhishi baada ya mashauriano hayo na makundi mengine.
Hamas imetoa kauli hiyo wakati Rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa anatarajia uamuzi wa Hamas kuhusu pendekezo la mwisho la kusitisha vita litatolewa ndani ya saa 24.