Kundi la kwanza la Waafrika kusini wazungu lawasili Marekani
12 Mei 2025Matangazo
Kundi la kwanza la Waafrika kusini wazungu 49, waliodai kubaguliwa kutokana rangi yao na kisha kupewa hadhi ya ukimbizi nchini Marekani chini pendekezo la rais Donald Trump,wamesafiri kuelekea Marekani.
Ndege iliyowabeba Waafrika kusini hao wazungu wa jamii ya kabila la Afrikaans,ambao wengi asili yao ni walowezi wa Kidachi, imewasili Washington leo Jumatatu majira ya asubuhi kwa saa za Marekani.soma pia:Marekani kuwapa makazi Waafrika Kusini weupe
Hatua ya Marekani ya kuwapokea raia hao waafrika Kusini inaongeza msuguano kati ya mataifa hayo mawili. Marekani inadai sheria mpya ya ardhi ya Afrika Kusini inawabagua wazungu.
Afrika Kusini imesema Marekani imejiingiza kwenye suala la ndani la kisiasa la nchi yake ambalo hailifahamu.