MigogoroIsrael
Hamas lasema liko tayari kwa mazungumzo ya amani
26 Aprili 2025Matangazo
Afisa wa kundi hilo la Kipalestina ameliambia shirika la habari la AFP lakini kwa sharti la kutotambulishwa, wakati ujumbe wa kundi Hamas ukijiandaa kukutana na wapatanishi mjini Cairo baadaye hii leo.
Aprili 17, Hamas, ambayo inapinga makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye baadhi ya maeneo, ilikataa pendekezo la Israeli lililojumisha usitishaji wa vita kwa siku 45, ili mateka 10 walio hai warejeshe.
Kundi hilo mara kwa mara limekuwa likidai kwamba makubaliano ya usuluhishi lazima yamalize vita, Israel iondoke kikamilifu kwenye Ukanda wa Gaza, kubadilishana wafungwa na misaada ya kiutu kuingizwa mara moja kwenye eneo hilo lililokumbwa na vita.