MigogoroMashariki ya Kati
Kundi la Hamas laridhia kuwaachia mateka 10 wa Israel
10 Julai 2025Matangazo
Hatua ya Hamas ni sehemu ya makubaliano ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kwa siku 60 huko Gaza baada ya Israel kuonyesha matarajio ya kufikiwa kwa mpango huo.
Mjumbe maalum wa Marekani huko Mashariki ya Kati Steve Witkoff amesema sehemu ya mpango huo itakuwa ni kuwarejesha mateka 10 walio hai . Hata hivyo Hamas wanaendelea kushinikiza kwamba Israel inatakiwa kuviondoa vikosi vyake vyote huko Gaza.
Wakati vita vikiendelea, na watu 26 wakiripotiwa kuuawa Gaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar amesema makubaliano hayo ya muda yanaweza kupelekea pia kufanyika mazungumzo mapana ya amani ya kudumu huku Rais Isaac Herzog akiitaja hiyo kuwa "fursa ya kihistoria" kuelekea mabadiliko.