Kufungwa kwa lango la Hormuz kutaathiri vipi uchumi duniani?
UchumiIran
Josephat Charo23 Juni 2025
Bunge la lran limeidhinisha kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz. Je vita hivi kati ya Israel na Iran na kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz kunaweza kuwa na athari gani kiuchumi? Josephat Charo alizungumza na Nasoro Kitunda, mchambuzi wa masuala ya uchumi aliyeko Dar es Salaam, Tanzania aliyetoa mtizamo wake kuhusu hatua hiyo.