MigogoroUrusi
Kremlin:Mkutano wa Putin na Trump utakuwa wa manufaa makubwa
13 Agosti 2025Matangazo
Kaimu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi. Alexei Fadeyev amesema mjini Moscow kwamba mkutano huo wa Ijumaa na unaosubiriwa kwa hamu utagusia masuala yote muhimu kuanzia mzozo nchini Ukraine hadi vizuizi vya mazungumzo ya kawaida kati ya mataifa hayo mawili.
Anatoa matamshi hayo wakati Trump akifanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na viongozi wa Ulaya wanaotaka kumshinikiza Trump kuhusiana na makubaliano ya maeneo. Kuna wasiwasi kwamba Trump anaweza kuingia makubaliano na Putin yatakayokiuka uhuru wa Ukraine.
Tangu ilipoivamia Ukraine mwanzoni mwa mwaka 2022, Urusi tayari imechukua mikoa minne ya Ukraine ya Luhansk, Donetsk, Zaporizhzhya and Kherson.