Kremlin: Putin yuko tayari kujadili mazungumzo ya amani
20 Julai 2025Matangazo
Peskov amesema kwa sasa dunia imeshazoea maneno ya rais wa Marekani Donald Trump ambayo wakati mwingine ni makali lakini pia akasisitiza kuwa Trump aliahidi kuendelea kutafuta makubaliano ya amani huku akitahadharisha kwamba ni "hatua inayohitaji uvumilivu na isiyo rahisi."
Urusi yapuuzilia mbali vikwazo vipya vya EU
Awali rais Trump alitangaza msimamo mkali dhidi ya Urusi na kuahidi kuipa Ukraine usaidizi wa kijeshi ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot.
Trump aliipa Urusi siku 50 za kukubaliana na mpango wa usitishaji mapigano au iwekewe vikwazo zaidi.