Kremlin: Putin na Zelensky hawawezi kukutana kwa sasa
25 Julai 2025Msemaji wa Ikulu hiyo Dmitry Peskov amesema mkutano huo sio rahisi kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti kama Ukraine ilivyopendekeza.
Amesema Urusi haiwezi kukubali mkutano huo kufanyika kabla ya makubaliano ya kina ya usitishaji mapigano.
Insert Peskov "Mkutano wa kilele unaweza na unapaswa kuweka hoja ya mwisho katika makubaliano ya kusitisha vita na kuweka wazi mbinu na makubaliano yanayopaswa kukubalika katika mchakato mzima unaoendeshwa na wataalamu. Haiwezekani kufanya kinyume ya hicho. Inawezekana kweli kupitia mchakato huo mgumu na mrefu kwa siku 30? Kwa kweli haiwezekani."
Urusi yaishambulia miji mitatu ya Ukraine wakati yakitarajiwa mazungumzo ya amani
Ukraine inaendelea kusisitiza kuwa viongozi wa mataifa hayo hasimu ni lazima wakutane kwanza ili kupiga hatua katika mchakato wa amani unaojikokta. Pande hizo mbili zimekutana mara tatu mjini Istanbul Uturuki ikiwa ni juhudi za kujaribu kufikia makubaliano ya kusitisha vita vilivyoanza February 24 wakati Urusi ilipomvamia kijeshi jirani yake Ukraine.