Kremlin yasema hakuna mipango ya Putin kuzungumza na Trump
29 Mei 2025Matangazo
Hivi Karibuni Trump ameonesha hadharani kukasirika kwake na rais huyo wa Urusi, akionya wiki hii kwamba Putin anacheza na moto kwa kukataa kujihusisha na mazungumzo ya kusitisha mapigano na Ukraine, huku vikosi vyake vikiendelea kupata ushindi katika uwanja wa mapambano.
Licha ya kauli hiyo ya Trump, Kremlin ilisema jana kwamba kipaumbele cha rais Putin ni matakwa ya taifa lake kuliko kitu kingine chochote.
Urusi yapendekeza mazungumzo mapya na Ukraine
Kuhusu kufanyika kwa mazungumzo ya amani, Urusi ilisema bado inaisubiria Ukraine kuweka wazi, iwapo itahudhuria mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika mjini Istanbul siku ya Jumatatu, baada ya Kyiv kutaka Moscow itume masharti yake ya amani kabla ya kukubali kuhudhuria.