Bado tunashirikiana na Marekani suluhu ya Ukraine - Kremlin
1 Aprili 2025Matangazo
Msimamo huo wa Urusi unakuja licha ya kauli ya Rais Donald Trump kwamba amekerwa na Rais Vladimir Putin.
Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, amewaambia waandishi wa habari kwamba Moscow inaendelea kushirikiana na Washington na kwamba Putin yuko tayari kuwasiliana na Trump.
Siku ya Jumatatu, Trump alikiambia kituo cha televisheni cha NBC kwamba amekasirishwa sana na Putin kukosoa uhalali wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, huku akitishia kuwawekea wanunuzi wa mafuta ya Urusi ushuru wa hadi asilimia 25 mpaka 50.