MigogoroUlaya
Kremlin: Urusi imezoea kuishi chini ya vikwazo
30 Julai 2025Matangazo
Hayo ni baada ya Trump kusema siku ya Jumanne kuwa Marekani itaiwekea Urusi vikwazo vya kiuchumi ikiwa ni pamoja na ushuru mkubwa, kama ndani ya siku 10 Urusi haitoonyesha maendeleo yoyote katika kuvimaliza vita vya miaka mitatu nchini Ukraine.
Hayo yanaarifiwa wakati pande hizo mbili zikiendelea kushambuliana vikali. Askari watatu wa Ukraine wameuawa na wengine 18 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la Urusi katika kambi ya mafunzo ya jeshi la Ukraine huko Honcharivske jimboni Tchernihiv. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imedai kuwaua au kuwajeruhi takriban askari 200.