MigogoroUlaya
Urusi: Viongozi 29 wa kigeni kuhudhuria sherehe za Ushindi
6 Mei 2025Matangazo
Miongoni wa viongozi hao ni pamoja na rais wa China Xi Jinping na Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil. Mshauri katika Ikulu ya Kremlin Yuri Ushakov amesema pia kuwa wanajeshi kutoka nchi 13 ikiwa ni pamoja na China, Misri na Myanmar, wataandamana katika gwaride hilo.
Hayo yanajiri wakati mapigano kati ya Urusi na Ukraine yanaendelea. Jeshi la Ukraine limefanya mashambulizi makubwa ya droni zaidi ya 100 na kuulenga mji mkuu Moscow ambapo viwanja 13 vya ndege ikiwa ni pamoja na vinne vya kimataifa karibu na Moscow vikilazimika kusitisha shughuli zake kwa muda.
Shambulio hilo linatishia mpango uliotangazwa na rais wa Urusi Vladimir Putin wa kusitisha mapigano nchini Ukraine kwa siku tatu kuanzia Mei 8 mwaka huu.